TIMU YA TAIFA (WANAUME) WAVU WA UFUKWENI, KUSHIRIKI KOMBE LA AFRIKA NCHINI MOROCCO, KUTAFUTA NAFASI YA KUSHIRIKI MICHEZO YA OLIMPIKI 2021.

Chama cha Mpira wa Wavu Nchini – TAVA, Tunayo furaha kuufahamisha uma kuwa timu yetu ya Taifa ya wannaume ya wavu wa ufukweni, imeingia kambini rasmi Jumatatu tarehe 7/6/21 Katika Hotel ya Golden Park ilioko Sinza, kumekucha, na itaanza mazoezi yake rasmi siku ya jumatano tarehe 9/6/21 katika fukwe za AZURA mjini Dar es salaam.